- Research Article
- 10.37284/jammk.8.2.3932
Usawiri wa UKIMWI kama Suala Mtambuko Katika Matini Teule za Fasihi ya Kiswahili ya Watoto
- Nov 10, 2025
- East African Journal of Swahili Studies
- Reuben Mwilaria
Fasihi ya Kiswahili ya Watoto imechangia katika kuangazia masuala mtambuko kama vile janga la UKIMWI, dhuluma za kijinsia na dawa za kulevya yanayoathiri afya ya binadamu na kutatiza kuafikiwa kwa maendeleo endelevu katika jamii. Makala hii ililenga kuchunguza usawiri wa suala la UKIMWI kama suala mtambuko katika matini teule za Fasihi ya Kiswahili ya Watoto. katika kuhamasisha jamii dhidi ya visababishi na athari zaKIMWI katika maisha ya binadamu. Malengo yafuatayo yaliongoza utafiti huu: Kutathmini nafasi ya Fasihi ya Kiswahili ya Watoto katika kuhamasisha jamii dhidi ya visababishi na athari ya ugonjwa wa UKIMWI na kubainisha njia mwafaka za kukabiliana na maambukizi na maenezi ya UKIMWI kama ilivyosawiriwa katika matini teule za Fasihi ya Kiswahili ya Watoto. Matini zilizochanganuliwa ni: Siku ya Ukimwi (John Kobia, 2008), Sitaki Iwe Siri (Bitugi Matundura, 2008), Madhila ya Bi. Shufaa (Nuhu Bakari, 2008), Pendo katika Shari (Clara Momanyi, 2008), Kosa la Marehemu (Andrew Panja, 2010) na Nimefufuka (Rebecca Nandwa, 2011). Matini teule zimo katika msururu wa “Afya Yangu.” Nadharia ya Uhalisia iliongoza utafiti huu. Sampuli ya utafiti iliteuliwa kimakusudi na data ikachanganuliwa kwa njia ya maelezo. Utafiti huu ulibainisaha kuwa Fasihi ya Kiswahili ya Watoto ilitumika kikamilifu kuhamasisha wanajamii kuhusu visababishi vya UKIMWI, athari zake na jinsi ya kuziboresha. Utafiti zaidi ulipendekezwa kuhusu nafasi ya Fasihi ya Watoto katika kukabiliana na dawa za kulevya. Hii ni kwa sababu vijana wamejihusisha na matumizi ya dawa za kulevya na kusababisha vifo na uharibifu wa rasilimali kama vile kuchoma shule na kuongezeka kwa utovu wa nidhamu. Kwa ujumla, utafiti huu umedhihirisha umuhimu wa fasihi ya Kiswahili ya Watoto katika kukabiliana na matatizo yanayokumba jamii kama vile changamoto za UKIMWI na namna ya kuziboresha ili kuafikiwa kwa maendeleo endelevu
Read more